Social Icons

Featured Posts

Wednesday, April 24, 2013

ADMIN PETTER ISUTI MIOYO KAFIWA NA BABA YAKE.

{RIP  Mzee Charles Chacha kaungane na kaka zako Mioyo Chacha na Silas Chacha}.. Haya ni maneno ya Admin. Nasi kama wana chama tuko nyuma yake katika kipindi hiki kigumu. R.I.P

Sunday, March 17, 2013

HAWA NDIYO VIONGOZ WAPYA

 Huyu anaitwa YUSUPH PIUS ni Mwenyekiti mpya wa MNH
 Huyu anaitwa GEORGE MASHIGILA ni Katibu mpya wa MNH.
 Huyu anaitwa LUCY PETER MAHUMBI ni Muhasibu mpya wa MNH.

Sunday, November 18, 2012

Ifuatayo ni habari fupi ya mazishi ya Mzazi wa mwanachama mwenzetu.

Ilikuwa ni huzuni kubwa kwa familia ya MARIAM THOMAS baada ya kuondokewa na Baba yake Mzazi.
Vile vile ni pigo kubwa kwa wana chama wote wa MNH

  Mwili wa marehem ulikuwa tayari kwaajili ya kuhifadhiwa katika nyumba ya milele.
 Baada ya mwili wa marehemu kuhifadhiwa na mashada kuwekwa na familia husika pamoja na watu wa karibu, watu walikusanyika kwaajili ya kufanya maombi ya mwisho.

Hii ni hali iliyo pelekea kipenzi wetu Mariam Thomas aliye fikwa na msiba kupoteza fahamu baada ya baba yake kipenzi kuhifadhiwa katika makaburi ya Misungwi.
MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEM MAHALI PEMA PEPONI {amina}
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA...

Friday, November 16, 2012

Mwana chama wa MNH Mariam Thomas kafiwa na Baba yake Mzazi.

Wana MNH, Jamani mwana chama mwenzetu MARIAM THOMAS amefiwa na Baba yake usiku wa kuamkia leo,
Hii ni siku ya majonzi kwetu na huu ni msiba wetu sote wana MNH.

Tuwe pamoja kwenye shida na Raha na hii ni sehemu moja wapo ya kutoa msaada na vile vile kuiliwaza familia nzima ya MARIAM THOMAS.
Mwili wa marehem umehifadhiwa kwenye hospitali ya rufaa ya Bugando.

kwa ujumla tujitahidi kumliwaza mwenzetu/ ndugu yetu katika wakati huu mgumu wa kuondokewa na Baba yake mzazi.
                     Afisa Habari MNH ♥ Issa Dody ♥

Wednesday, November 7, 2012

MWANZA NDIYO HOME yapata viongozi wapya

Bw.Swahiba Machozi-Katibu mkuu
Siku ya jumapili tarehe 4/11/2012 tuliendelea na kikao chetu kwa mujibu wa katiba,ambayo hutuelekeza kufanya kikao kila jumapili ya mwanzo wa mwezi. 
Kikao chetu kilianza majira ya saa kumi na nusu kutokana na hali ya hewa iliyokuwepo.Wajumbe hawakuwa wengi sana,lakini naamini kuwa wale waliofika siku hiyo ndio wanachama hai.

Tulikuwa na ajenda kama tano ambazo mwenyekiti aliziwakilisha kwa niaba ya makatibu ambao hawakuwepo.

Ajenda zilikuwa ni:
- Kufungua kikao
-Mabadiliko ya Ada
-Uteuzi wa Makatibu wapya
-Ununuzi wa simu ya kikundi
- Mengineyo
- Kufunga kikao.

Bi Happy James- Katibu msaidizi
Baada ya mwenyekiti kufungua kikao,alifafanua hoja ya mabadiliko ya Ada kutoka shilingi 2000 hadi shilingi 10000 kwa mwezi.Hii ni kutokana na umuhimu wa mambo tunayotakiwa kuyafanya,pia kutokana na kushuka sana kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.
Tuliona kwamba kuendelea kutoa Tsh 2000 kwa mwezi hatutaweza kufikia malengo tuliyapanga.
hivyo kila mwanachama ni lazima alipe shilingi 10000 ambayo ni Ada ya kila mwezi.

Pia kutokana na kuongezeka kwa Ada,pia gharama za kujiunga na Mwanza Ndiyo Home kwa mwanachama mpya zilipanda kutoka shilingi 5000 ya awali hadi shilingi 50000.

Kutokana na makatibu ambao tulikuwa tumewachagua hapo awali kutotimiza wajibu wao,tuliamua kuteuwa makatibu wapya,ambapo Bwana Swahiba Machozi aliteuliwa kushika nafasi ya katibu mkuu ambayo ilikuwa ikushikiliwa na Richard Saiya. Pia Bi Happy James aliteuliwa kuwa katibu msaidizi nafasi iliyokuwa ya Samson Simon.

Bw.Issa Dody- Afisa habari
Pia kutokana na umuhimu wa kundi letu,tuliongeza nafasi moja ya Afisa habari ambaye atakuwa anahusika na taarifa zote zile zinazohusu kikundi chetu.Kazi yake kubwa ni kutoa taarifa pale inapohitajika.Nafasi hiyo ilienda kwa Issa Dody,ambapo ili kumuwezesha kufikisha habari kwa haraka,tulichanga pesa ya kununulia simu atakayoitumia kwa matumizi ya kikundi pekee.

Katika mengineyo,wanakikundi walishauri wanakikundi ambao sio hai,hawajishughulishi na shughuli yoyote ile ya kundi,waangaliwe upya.
Pia kamati tendaji itakuwa ikikutana siku moja kabla ya kikao ili kuandaa ajenda za siku ya kikao.

Mwisho mwenyekiti alifunga kikao,kwa kuwashukuru wote waliofika kikaoni.