Social Icons

Saturday, November 3, 2012

TAARIFA KWA WANACHAMA WOTE

Kwanza napenda nichukue nafasi hii kuwashukuru wanachana wote wa MNH kwa ushirikiano wao waliouonyesha kwa wenzetu ambao walipatwa na msiba.Jambo hili linaashiria mambo mazuri hapo baadae.

Najua tunakabiliwa na changamoto nyingi kwenye umoja wetu,lakini kwa nia ya dhati tuliyo nayo naamini tutafanikiwa na kufikia malengo tuliyoyaweka.Yatupasa tushirikiane kwa hali na mali ili tuhakikishe tunatimiza yale yote tunayotaka kuyafanya.

Pia napenda niwakumbushe wanachama wote kuwa,kesho tarehe 4/11/2012 tutakuwa na kikao pale Bugando Hill kitakachoanza saa 9:30 jioni. Unaombwa sana ufike kwani kuna mambo mengi tunayotaraji kuyafanya na kuzungumza kesho.Moja kati ya yote hayo ni kupata picha ya kila mwanachama ili iweke kwenye albam yetu ya hapa kwenye blog.

Mwisho niwatakie mapumziko mema ya mwisho wa wiki.

Imetolewa na:
Dk Syaga James
MWENYEKITI

0 Maoni yako:

Post a Comment